Duration 12:29

Je Vifaa gani huhitajika wakati wa Kujifungua | Maandalizi ya Kujifungua kwa Mjamzito.

42 163 watched
0
489
Published 18 Jul 2021

Mjamzito anatakiwa kujiandaa Kisaikolojia, Kibaologia na Kiakili kipindi ambacho tayari Mimba yake imefikisha Miezi Tisa na muda wa kukaribia kujifungua. Endapo Mjamzito alihudhuria Kliniki ipasavyo na kupewa elimu muhimu inayo husiana na Ujauzito, Tahadhari zakuchukua kipindi Cha Ujauzito na Maandalizi maalum kabla na baada ya kujifungua. Humsaidia kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kujifungua na kumpokea Mtoto wake atakayezaliwa. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya akina Mama huwa hawajiandai kikamilifu wanapokaribia kujifungua, Jambo ambalo huonekana ni la Dharula na kupelekea changamoto mbalimbali siku ya kujifungua Mimba zao. Pamoja na kwamba Mjamzito anatakiwa kujiandaa kikamilifu kuhusiana na Masuala ya Kisaikolojia, Kibaologia na Kiakili. Mjamzito anatakiwa kujiandaa kikamilifu katika Masuala yafuatayo: 1. USAFIRI Mjamzito na familia yake inatakiwa kuhakikisha kwamba kutakuwa na uwezekano wa kupata usafiri muda wowote siku ambayo Uchungu utaanza kwa ajili ya kuwahi Hospitali au kituo Cha Afya. Endapo Mjamzito anaishi kijijini na sehemu zisizo na Usafiri wa haraka hususani wakati wa Usiku, Mjamzito anatakiwa kuwa karibu na Zahanati au kituo Cha Afya muda mfupi kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifungua. 2. MSINDIKIZAJI. Mjamzito na Familia yake wanashauriwa kuwa na Mtu au Watu maalumu kwa ajili ya kumsindikiza wanapoelekea hospitali, Msaidizi huwa ni wamuhimu sana endapo itatokea dharula au Jambo lolote wakati Mjamzito akiwa katika safari kuelekea Kituo Cha Afya na nk. 3. MTU ATAKAYE BAKI NYUMBANI. Mjamzito na Familia yake wanatakiwa kuhakikisha kwamba kuna Mtu maalum atakaye bakia nyumbani, endapo Mume atamsindikiza Mjamzito, Anayebaki nyumbani hubaki kama Mlinzi na Mhudumu endapo kuna Watoto wadogo wamebaki nyumbani kipindi ambacho Mjamzito anaelekea hospitali. 4. VIFAA VYA KUJIFUNGULIA Mjamzito na Familia yake wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanavifaa maalum kwa ajili ya kujifungulia wawapo hospitali. Vifaa hivyo ni Kama. I. Begi kubwa #1. Hutumika kwa ajili ya kuhifadhia Vifaa vingine tajwa hapo chini. II. Mpira wa kujifungulia au Karatasi ya Nailoni#1. Hutumika kutandika kwenye Kitanda Cha kujifungulia. III. Mpira wa kuvaa Mikononi #10. Hutumika na Wahudumu kwa ajili ya kuvaa Mikononi kipindi cha kupima njia ya Mlango wa Uzazi na kukuzalisha. VI. Kibanio cha Kitovu #2. Hutumika kuzuia utokwaji wa Damu au kufunga Kitovu Kipindi cha kutenganishwa kwa Mtoto na Kondo la Nyuma. V. Kiwembe cha Upasuaji #2. Hutumika kukatia Kitovu wakati wa kutenganishwa Mtoto na Kondo la Nyuma na kukatia Nyuzi wakati wa kushonwa endapo Mjamzito amechanika wakati wa Kujifungua. VI. Nguo aina za Khanga zilizotumika #4. Hutumika kwa ajili ya kumvisha Mtoto Mara baada ya kujifungua, hapa unatakiwa kuwa na Khanga zilizotumika siyo mpya. VII. Nguo aina za Vitenge zilizotumika#4. Hutumika kwa ajili ya Mjamzito kujifunika na kutandika juu ya mpira uliowekwa Kitandani. VIII. Malapa au Ndala #1 Hutumika kipindi ambacho Mjamzito atahitaji kwenda Bafu au Choonk kabla au baada ya kujifungua anapokwenda kuoga. IX. Dishi #1 Hutumika kuweka Nguo zilizo loa au uchafu mwingine unapokuwa Wodini. X. Sabuni na Mafuta ya Mjamzito. Hutumika endapo Mjamzito atahitaji kujisafisha Mwili wake. XI. Pamba kubwa #1 XII. Nyuzi za Upasuaji # 1 Hii siyo lazima kwa sababu hospitali inaweza ikatumia Uzi wake endapo bahati mbaya umechanika na baada ya huduma utatakiwa kulipia au kurudishia baada ya kutumia. XIII. Pedi kubwa za Mjamzito Hii siyo lazima unaweza kutumia Khanga laini kwa ajili ya kuzuia Damu zinazotoka Ukeni Mara baada ya kujifungua. XIV. Mpira wa Mkojo#1 na kibegi chake #1. Mpira wa Mkojo huwa silazima sana, japokuwa huweza kutumia kwa baadhi ya Wajawazito na wanjifungua kwa Upasuaji,kwa ajili ya kuhakikisha Kibofu cha Mkojo kinakuwa tupu. XIV. Vifaa vya Mtoto. Mfano; Mafuta ya Nazi kwa ajili ya kumpakaa Mtoto,Kofia, Soksi, Pampasi na Babsho kwa ajili ya kumfungia Mtoto awe katika mazingira ya Joto, Leso laini za kumfutia Mtoto wakati wa kumsafisha na nk. 5. FEDHA. Mjamzito na familia yake wanatakiwa kujiandaa kikamilifu kuhusiana na Fedha au Kiuchumi endapo itatokea dharula yoyote hata kama amejiandaa Kisaikolojia, Kibaologia, Kiakili na Vifaa kama ilivyotajwa hapo juu. MUHIMU: Kujifungua siyo jambo la kushtukiza au Dharula, endapo wewe ni Mjamzito hata kama ulipata Mimba kwa bahati mbaya au Bila kupanga, imetokea kwa bahati mbaya basi hakikisha unanunua kitu kimoja kimoja au kidogo kidogo mpaka kufikia miezi 9, unakuwa tayari na vifaa vyote. Uendapo hospitali bila kujipanga au bila Vifaa huwa ni kikwazo kikubwa kwa watoaji wa huduma za kiafya kwa sababu hutengeneza mazingira magumu ya kazi zao. #DrMwanyika #MamaAfya #MaandaliziYaKujifungua

Category

Show more

Comments - 186