015-Nena Mungu
Speak To My Soul
Nena rohoni yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke."
'Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.
CHORUS
Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong'oneza kwa pole wa pendo:
"Daima utashinda, Uhuru ni wako."
Nisikie maneno: "Huachwi upweke."
Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.
Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yako tena, Daima 'kusifu.
Singers:
#UpendoMashika
#FadhiliMashika
○ PNFP OFFICIAL 2020